TANGAZO

TANGAZO

ALIYEIBIWA WATOTO WAWILI NA DADA WA KAZI AELEZEA JINSI ALIVYOWAPATA


Mohamed Kasim, Mkazi wa Tandika Temeke amelishukuru Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa namna lilivyofanikisha kuwapata watoto wake wawili mmoja mwenye umri wa miaka 5 na minne walioibiwa na dada wa kazi.

Jeshi la Polisi limesema lilianza upelelezi huo mara baada ya kubaini binti wa kazi za ndani kwa kushirikiana na mganga wa kienyeji walipanga njama za kuiba watoto hao ambao wamepatikana Januari 14, 2025 nyumbani kwa mtuhumiwa Abdulkarim Shariff (43) Mganga wa Kienyeji Mkazi wa Kimara Baruti Ubungo.


Aidha Jeshi la Polisi limeeleza kuwa Afya za Watoto hao baada ya vipimo vya Hospitali zipo vizuri.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema majojiano na watuhumiwa hao bado yanaendelea ili kubaini nini kiini cha malengo ya tukio hilo.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limetoa wito kwa wananchi kuepuka tabia ya kuchukua wasaidizi wa kazi za nyumbani wasiojua historia na tabia zao.



Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com