TANGAZO

TANGAZO

HABARI PICHA: POLISI SONGWE NA KAMPENI YA ' TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA'

Picha za matukio mbalimbali zikimuonesha Koplo Gladness Sizya kutoka Dawati la Jinsi na Watoto Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe akizungumza na Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza wa Shule ya Sekondari Nsenya baada ya kuwapa elimu ya madhara ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto ikiwa ni mwendelezo wa Kampeni ya TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA Januari 22, 2025.





Koplo Gladness baada ya kutoa elimu hiyo aliwataka wanafunzi hao wasifumbie macho vitendo hivyo pindi waonapo au wafanyiwapo na wasisite kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kushughulikiwa kwa haraka kwa manufaa ya masomo na maisha yao ya baadae.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com