TANGAZO

TANGAZO

WATAFUTA KAZI NJE YA NCHI ZINGATIENI SHERIA NA TARATIBU - WAZIRI RIDHIWANI KIKWETE


Na. Mwandishi wetu - Saudi Arabia

Serikali imekemea watanzania wanao kwenda kufanya kazi nje ya nchi bila kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa inasababisha kutojulikana walipo na shughuli wanazozifanya.



Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa makubaliano ya kuwezesha na kuratibu Ajira za Watanzania nchini Saudi Arabia leo Januari 27. 2024.



Aidha, amesema uhusiano mazuri uliopo baina ya Tanzania na nchi ya Saudi Arabia hawataruhusu wafanyakazi kufanya kazi au kusafiri bila kufuata utaratibu, hivyo kila mtanzania anayehitaji kufanya kazi nje ya nchi apitie kwa mawakala wanatambulika baina ya nchi hizo mbili.

Mhe. Ridhiwani amesema miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa watanzania kusafiri kwenda nchini Saudi Arabia, upimaji wa Afya zao, kupata kazi zenye staha na mshahara mzuri ambao utawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com