January 26, 2025
Waaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya São Tomé na Príncipe Mhe. Patrice Emery Trovoada amewasili nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ujulikanao kama #Mission300 utakaofanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Mhe. Trovoada amepokelewa na Trovoada amepokelewa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega na viongozi wengine Waandamizi wa Serikali.