TANGAZO

TANGAZO

WAZIRI KIKWETE AWASHUKURU WADAU WA MAENDELEO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amewashukuru wadau wa maendeleo kwa ushirikiano mzuri wanao uonesha kwa serikali.


Kikwete ametoa shukurani hizo wakati akichangia kwenye kikao maalum cha Mawaziri mbalimbali duniani (Ministerial Roundtable) katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu soko la ajira unaofanyik Jijini Riyadh nchini Saudi Arabia.



Akizungumzia wakati akichangia hoja iliyowasilishwa kuhusu maendeleo ya vijana na mabadiliko sasa, Kikwete alishukuru ushirikiano uliopo baina ya wadau wa maendeleo juu ya kazi wanaofanya bila kusahau miongozo na mabadiliko ambayo yamefanyika nchini Tanzania ikiwemo mikakati ya kukuza ujuzi, matumizi ya tehama, mkazo katika miradi inayotoa ajira nyingi na ile ya kimkakati. 

Mkutano huo unawakutanisha Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka nchi zaidi ya 45 duniani kujadili na kuweka mikakati ya kuongeza kazi za staha kwa vijana kwa kuzingatia mchango wa sayansi na teknolojia.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com