TANGAZO

TANGAZO

JESHI LA POLISI LAMKAMATA RAIA WA MALAWI NA VIPANDE 18 VYA MENO YA TEMBO


Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limemkamata mwanaume mmoja kwa tuhuma za kupatikana na nyara za serikali meno ya tembo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga alisema Februari 16, 2025 saa 04:30 usiku huko Kitongoji cha Msia, Kata ya Chitete, Tarafa ya Bulambya Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe.


 Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kupitia taarifa za kiintelijensia pamoja na misako na doria za mara kwa mara zinazoendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Idara mbalimbali ikwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA Wilaya ya Ileje limefanikiwa kumkamata Chisamba Siame Kameme (60) Mkukima, raia wa Nchi ya Malawi akiwa na vipande 18 vya meno ya tembo yenye thamani ya 84.2Kg.

Aidha baada ya kufanya tathimini na wataalam ilionesha kuwa thamani ya meno hayo ni kiasi cha Shilingi Milioni 153,540,000 (Milioni Mia moja Hamsini na Tatu Laki Tano na Arobaini Elfu) ikiwa ni sawa na Tembo wa 03 na kila tembo 01 akiwa na thamani ya 51,180,000 (Milioni Hamsini na Moja Laki Moja na Themanini Elfu) alivyokuwa ameviweka kwenye mfuko wa salfeti kisha kufunga kwenye baiskeli rangi nyeusi kwa lengo la kuviuza.

Aidha, Shauri la kesi hii upelelezi bado linaendelea na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi Mkoani Songwe, linatoa wito kwa baadhi ya mtu au watu wenye tabia ya kufanya uhalifu wa kijangili kwa wanyama pori ambao ni kinyume na sheria kuacha mara moja kwani halitosita kuwachukulia hatua wale wote wenye tabia kama hiyo ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani ili iwe fundisho kwa watu wengine.

 

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com