


Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais amesema Serikali, inashukuru kwa maisha ya mama Sekunda ambaye alimzaa na kumlea Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye amekuwa Mtendaji na Kiongozi mahiri katika utumishi wa umma, tangu alipokuwa anafundisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam na katika nafasi mbalimbali alizoshika Serikalini.


Makamu wa Rais amesema kila mmoja anapaswa kujitahidi kuishi vema na binadamu wenzake na kufanya kazi kwa bidii katika nafasi mbalimbali ili kutoa mchango mzuri kwa familia na Taifa, na kuacha historia nzuri na mifano bora ya kuigwa na jamii. Ameongeza kwamba ni muhimu kujiandaa kumrudia Muumba maana hakuna ajuaye siku wala saa.






Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
06 Februari 2025
Tarakea – Kilimanjaro.