Hafla ya msimu wa 35 wa mbio za Kili Marathon imefanyika Jana Februari 22, 2025 katika viwanja vya ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo benki ya CRDB imeendeleza udhamini wake wa mbio za Kilomita 5 zinazojulikana kama CRDB Bank 5km Fun Run. Kimsingi, huu ni mwaka wa pili mfululizo tangu benki hiyo ianze kufanya udhamini huo jambo ambalo limezifanya mbio hizo kuendelea kuwa na msisimko mkubwa na wa kipekee.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mbio hizo, Mkuu wa kitengo cha Masoko CRDB Bank Bi. Joseline Kamuhanda amesisitiza kuwa benki ya CRDB inafanya hivyo, kwasababu inatambua na kuthamini umuhimu wa michezo kwa afya na kipato kwa wananchi wakiwemo wateja wao ambao wanawajali sana.
Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com