Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Stephen Wasira, amewahakikishia wananchi mkoani Mara kuwa Chama kitaendelea kuzibeba changamoto zinazowakabili na kuendelea kuzitafutia ufumbuzi.
Miongoni mwa changamoto hizo ni ujenzi wa baadhi ya barabara ambazo zinapaswa kujengwa kwa lami ili kuzifungua baadhi ya wilaya za mkoa pia kuiunganisha Mara na nchi jirani ya Kenya kwa barabara za lami.

Wasira aliyasema hayo jana Rorya mkoani Mara alipokuwa akizungumza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Rorya.
“Sisi ni Chama Cha Mapinduzi, kazi yetu ni kusikiliza kero za watu, mnaweza tukacheza ngoma, lakini kama matatizo ya watu hayazungumzwi na hayatafutiwi ufumbuzi watu watakuwa hawana hakika kama Chama hiki kinashughulika na matatizo yao.
“Sasa nimemuelewa rafikiangu wa TANROADS tatizo lake la bajeti, anapewa sh. bilioni moja, kwa hiyo kama anatengeneza sana ni kilometa moja au moja na robo, na kwa kuwa barabara ina kilometa 56 maana yake ataikamilisha kwa miaka 56.
“Hilo ni tatizo la kibajeti ambalo inabidi kulifikisha kwa waziri anayehusika ili aone namna anavyoweza kusaidia kwa sababu jambo hili limeahidiwa na Marais watatu” alisema.
Barabara ziko nne katika mkoa wa Mara ambazo kwa bahati mbaya zote bado hazijakamilika kuna barabara inayokwenda Kilongwe, kuna barabara ya Tarime kwenda Serengeti, kunabarabara ya kutoka Sanzati-Nata-Mugumu na tuna barabara inayotoka Musoma kwesigasi.
Kilongwe, umepita umeiona mwenyewe, barabara kwetu ni changamoto watu wa Rorya tunaomba barabara hii kwa kuwa ni ,uhimu kwa uchumi wa wananchi wa Rorya,”

