
Vyombo vya habari Nchini vimetakiwa kusimamia haki na Usawa katika kuhabarisha Taifa mwenendo wa Kampeni za vyama vya siasa pamoja na kumzingatia weledi na kanuni za Utangazaji.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Habari,Utamaduni , Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Watoa huduma za Utangazaji unaofanyika Februari 13 Hadi 14,2025 Jijini Dodoma.
Amesema kuwa inafaa kwa washiriki wote kufahamu kuwa wanazielewa Sheria na kanuni zote zinazosimamia uchaguzi mkuu Nchini ili kuweza kutoa ripoti zenye haki na Usawa kwa jamii.
Amesema kuwa ni matarajio yake kuona zitakazowasilishwa kwenye Mkutano huo zinazolenga kukumbushana wajibu wa vyombo vya habari kuelekea uchaguzi Mkuu ili Wananchi waweze kuelimika na kufanya maamuzi sahihi katika kipindi Cha uchaguzi.
Ufunguzi huu umehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA, Jabiri Bakari.
