Mbunge wa Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga pamoja na wanawake wa Kijiji cha Tandala Kikundi cha Super Woman leo Machi 7, 2025 Asubuhi wameamkia Kijiji cha Ihela kwenda kumuona Bi. Amenipa Mahenge ambaye anachangamoto ya miguu.
Ikiwa hii ni wiki ya Mwanamke iliyoambatana na kutenda matendo mema kwa wenye uhitaji.
Mbunge wa Makete Sanga amemuombea Bi Amenipa na kusema " kama Mungu aishivyo tunawaombea wote wenye uhitaji wauone mkono wa Bwana".
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kimkoa (Mkoa wa Njombe) yatafanyika Wilayani Makete yenye Kaulimbiu isemayo "Wanawake na Wasichana 2025;
Tuimarishe Haki, Usawa na uwezeshaji.
![]() |

















