Matukio katika picha kabla na wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kinachoendelea muda huu Makao Makuu ya Chama hicho Mikocheni Dar es salaam.
Kikao hicho kinaongozwa na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, hii ni baada ya mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. John Heche asubuhi ya leo kwenda katika viwanja vya Karimjee kumuaga Prof. Philemon Sarungi. Baada zoezi hilo watafika Makao Makuu ya Chama hicho kuendelea na kikao.
![]() |




















