Maafisa Kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Afisa Uhifadhi Mkuu- Masoko, Michael Makombe (wa kwanza kulia) pamoja na Afisa Uhifadhi Mwandamizi- Uhusiano wa Umma, Kassim Nyaki (wa pili kutoka kulia) wameshiriki kipindi mubashara kupitia TBC Safari Channel na Bongo FM kuelezea upekee wa vivutio vya utalii vilivyoko hifadhi ya Ngorongoro, gharama za kuingia kutalii Ngorongoro, shughuli ambazo wageni wanaweza kuzifanya wakiwa ndani ya hifadhi na kuelezea namna NCAA inavyoshirikiana na wadau mbalimbali katika kuhusianisha utalii na michezo (Sport Tourism).