Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufani Mh. Jacobs Mwambegele ameagiza kuongeza vifaa vya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye vituo vya Uandikishaji vyenye watu wengi.
Jaji Mwambegele atoa maagizo hayo wakati akikagua mwenendo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari na kubaini uwepo wa ongezeko la watu wengi kwa baadhi ya vituo katika Mkoani Dar Es Salaam.
![]() |
Mwamko wa watu kujitokeza kujiandikisha unazidi kuongezeka katika halmashauri za mkoa wa Dar Es Salaam ambapo Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mh BALOZI OMAR RAMADHAN MAPURI akiwa halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ameshuhudia ongezeko hilo vituoni.
Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri la Jiji la Dar Es Salaam Wakili FARAJA NAKUA akazungumzia zozi hilo la Uboreshaji katika halmashauri yake huku akisisitiza wenye sifa kutoikosa fursa hiyoya kujiandikisha ili washiriki kuchagua viongozi muda wa uchaguzi utakapofika.
Wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam waliozungumza na Uchaguzi TV wameonesha kufurahishwa kwao na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuendesha zoezi hili pamoja na hatua za haraka zilizochukuliwa kuongeza vifaa vya Uboreshaji.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliloanza Machi 17 unatarajiwa kukamilika Machi 23 kwa halmashauri za mkoa wa Dar Es Salaam ambapo vituo vimewekwa kwenye mitaa na vinafunguliwa kuanzia saa 2 kamili asubuhi na vinafungwa saa 12 ka,mili jioni Kauli Mbiu Inasema KUJIANDIKISHA KUWA MPIGA KURA NI MSINGI WA UCHAGUZI BORA







