-Ni kuelekea mchakato wa kupata wagombea ubunge ndani ya Chama
-Asema taarifa zao anazo, awataka waache kujihusisha na rushwa
-Atoa rai kwa wajumbe wapiga kura kuwa huru kuchagua watu sa
Makaku Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema anazo taarifa za baadhi ya wanachama wanaotaka ubunge kuanza kunja maadili katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Hivyo amewakumbusha wanaotaka ubunge na wabunge waliopo, kuzingatia maadili huku akitoa rai kwa wajumbe wa Chama ambao watapiga kura kuchagua mgombea mmoja kati ya watatu ndani ya Chama kuhakikisha wanapiga kura kwa uhuru bila kupewa fedha na wataka ubunge.
Akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi katiKa kikao cha ndaani kilichofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera jana, Wasira alisema Chama kimebadilisha utaratibu wa kupata wajumbe wanaopiga kura kupata wagombea wake.
“Huko nyuma hapa Ngara waliokuwa wanapiga kura ni wajumbe 700, lakini kwa sasa ni zaidi ya 10,000 ni wengi maana sasa hivi mabalozi wote wanapiga kura, kwenye kamati zenu za watu wanne kote huko wanapiga kura.
“Kamati za jumuiya zote zinapiga kura, kamati zao za utekelezaji zote zinapiga kura na watu wengine wengi ambao siwezi kuwataja wote. Tunachotaka mjue sababu za mabadiliko hayo kwanza tunatanua demokrasia ndani ya Chama chetu.
“Pia tunataka watu wengi wanaopiga kura watuambie kwa maoni ya wananchi wa Ngara mtusaidie kusema katika watu watatu mmoja katika hawa anamzidi mwengie ili tupate mtu wa kupeperusha bendera ya CCM kati ya hawa watatu, tujue wananchi wanasemaje,” alisema Wasira.
Alifafanua yeye ni Makamu Mwenyekiti na moja ya kazi yake ni kusimamia maadili hususan kwa wanaotaka ubunge kwani wapo ambao wameanza kunyemelea na wananyemelea kwa kuvunja maadili.
“Wajumbe tunataka mpige kura mkiwa watu huru muiambie CCM mkimsimamisha huyu tutashinda bila tabu kama atakavyoshinda Dk. Samia. Naamini kazi hii wajumbe mnaiweza vizuri hivyo tuleteeni wagombea wanaokubalika.
“Lakini wale wanaotaka ubunge baadhi yao nina habari zao wameanza kuvuruga maadili wanataka muwapigie kura kwa hela wanazowapa na Biblia inasema rushwa inapofusha maana yake ni kwamba ukiona mtu anasambaza hela lazima ujiulize kwani hiyo imekuwa huduma?.
“Na hili nalisema kwa wagombea wapya na wabunge waliopo tunachunguza tunajua mwenendo huo, sasa nawaambia acheni kupofusha wajumbe, na ninyi wajumbe na mabalozi wa nyuma 10 mtupe heshima ya kutuletea watu wazuri, ndio wajibu wenu,” alieleza.



