TANGAZO

TANGAZO

WASIRA ATOA MAELEKEZO KUSAIDIA WANANCHI MGOGORO WA MBARALI

 



Na Mwandishi wetu Mbarali.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeielekeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Juma Homera kuweka utaratibu mzuri wa kugawa sehemu ya ardhi kwa wananchi wa Mbarali itumike kwa shughuli za maendeleo  hususan kilimo.


Hatu hiyo imetokana na malalamiko ya wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambao wamesema wanashindwa kufanya shughuli za kilimo baada ya kuondolewa na serikali kupisha hifadhi ya Mto Ruaha, hivyo kuwasababishia hali ngumu ya uchumi na maisha.


Maelelekezo hayo yametolewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipokuwa akizugumza na wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya katika mji wa Ubaluku.



“Nimewasikiliza wananchi wa Mbarali kuhusu huu mgogoro wa ardhi, tumesikia kilio chenu na kazi yetu kubwa CCM ni kushughulika na matatizo ya watu. Mmezungumza kuhusu GN 28 ambayo hii tayari imefutwa maana ilinung’unikiwa na watu wote wa Mbarali.


“Hatuwezi kubaki nayo lakini Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake alishaiondoa GN 28 ambayo ilikuwa imechukua vijiji 32 na kuwa sehemu ya hifadhi ya Mto Ruaha, sasa kuna GN 754 ambayo hii imeondoa vijiji 28 katika hifadhi na kuvirejesha kwa wananchi na vijiji vitano ambavyo vimebaki hifadhini vinaendelea kufanyiwa kazi,” amesema.



Awali Mbunge wa Mbarali, Bahati Ndingo akuzungumza katika mkutano huo, aliiomba serikali kuwafikiria wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwa idadi yao ni kubwa na eneo wanalolitumia kwa shughuli za kilimo ni dogo hivyo aliomba wamegewe eneo lingine wafanye shughuli zao.


“Kwa mujibu wa sensa yam waka 2022 Mbarali ina watu 400,000, pia tunapokea wageni wengi wanakuja kufanya shughuli za maendeleo. Ni wilaya ya saba kwa mifugo mingi Tanzania, kuna migogoro mikubwa kati ya wafugaji na wakulima.

“Ushauri wetu habari ya maendeleo ambayo yamefanywa na Rais Samia hapa Mbarali hakuna mwenye shaka, umeme vijiji vimepata umeme, vitongi 518 vimepata umeme, anastahili pongezi kubwa,”



Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com