Picha za matukio mbalimbali yakimuonesha Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban akiwa amemtembelea askari Konstabo Yusuph Mapuli nyumbani kwake Aprili 17, 2025 ambaye anasumbuliwa na mguu ambao alipata ajali katika majukumu ya kazi za kila siku.
ACP Akama katika hatua hiyo ya kumfariji askari huyo aliambatana na Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Songwe Mrakibu wa Polisi (SP) Tukae Kirungi kwenda kumfariji Askari huyo ili apate faraja na kuona yupo pamoja na wafanyakazi wenzake na viongozi wake katika ngazi ya Mkoa.
Kwa upande wake Askari huyo amewashukuru viongozi hao kwa kujitoa na kwenda kumfariji sambamba na kumuombea nafuu ili aweze kurejea kwenye majukumu yake ya kazi.



