TANGAZO

TANGAZO

AJALI YATOKEA MWANGA, YAUA 7 WENGINE WAJERUHIWA



Na rechal kimath - Kilimanjaro

Watu saba wamefariki dunia kwa ajali ya gari lenye namba za usajili T. 222 DNL Bus Yutong Kampuni ya Mvungi ikitokea Ugweno kwenda jijini Dar es salaam eneo la kijiji cha Mamba Msangeni kata ya Msangeni Wilaya ya Mwanga baada ya basi hilo kuacha barabara na kupinduka kwenye bonde.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo alhamisi Aprili 03, 2025 na Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro imesema kuwa Kati ya hao waliofariki ni wanaume wawili na wanawake watano akiwemo mtoto wa miaka miwili na majeruhi 42 na kwamba ilitokea majira ya saa Kumi na Mbili na dakika arobaini na tano asubuhi April 03, 2025.




Majeruhi wote wanaendelea na matibabu Hospitali ya Kifula, Hospitali ya Wilaya ya Mwanga, Hospitali ya KCMC Moshi na Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi.


Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kulimudu gari wakati anapishana na gari jingine kwenye kona kali na kuacha barabara na kutumbukia bondeni.


Dereva wa gari hilo anashikiliwa kwa mahojiano Zaidi


Majina ya Waliofariki ni Ashura Omari Sakena (47), mkazi wa Vuchama Mwanga, Zaituni Hashimu Mwanga (52), Mkazi wa Masumbeni Mwanga, na Halima Omari (02), Mkazi Mwanga,


Wengine ni Judithi Safieli mkazi Mwanga, (43), Mkazi wa Mangio Mwanga, Benadetha (20), Mfanya kazi wa ndani, Mkazi wa Ugweno, Haji Abubakari, (50), mkazi wa Kifula na . Hamadi Hussein Mshana (64), mkazi wa Ngalanga Ugweno.


Miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya Wilaya ya Mwanga kusubiri uchunguzi na taratibu zingine.




Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com