TANGAZO

TANGAZO

DKT. BITEKO AWASILI MKOANI IRINGA

 


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Aprili 26, amewasili mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ya siku moja. 


Katika Uwanja wa Ndege wa Nduli, Dkt. Biteko amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Peter Serukamba


Akiwa mkoani humo anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za kuwekwa wakfu Askofu Mteule Romanus Elamu Mihali kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa.



Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com