TANGAZO

TANGAZO

EKARI 41 ZATENGWA KWA AJILI YA OFISI ZA TANAPA ENEO LA KANZUNGU BUNDA

 


Na. Anangisye Mwateba-Bungeni Dodoma


Wizara ya Maliasili na utalii, kupitia shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 41.13 katika eneo la Kunzugu, Kata ya Balili, Mjini Bunda kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za TANAPA Kanda ya Magharibi.


Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) alipokuwa akijibu swali la Mhe. Robert Chacha Maboto aliyetaka kujua Serikali itajenga lini Makao Makuu ya TANAPA katika Halmashauri ya Mji wa Bunda.


Aidha Mhe. Kitandula aliongeza kuwa Serikali imekamilisha zoezi la upembuzi yakinifu na uandaaji wa michoro kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo. Kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza kwenye mwaka wa fedha 2025/2026.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com