![]() |
Janeth Thomson Mwambije, Ni Mzaliwa Wa Ukonga, Wilaya Ya Ilala, Mkoa wa Dar Es Salaam. Mwenye Asili Ya Mbeya.
ELIMU
Alifanikiwa Kuhitimu Shahada Ya Kwanza Kwenye Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Baada Ya Kuhitimu Elimu Ya Juu Ya Sekondari (Advance) Kwenye Shule Ya Wasichana, Premier.
SAFARI YAKE YA KISIASA
Janeth Thomson Mwambije Alianza Uongozi Akiwa Katika Shule Ya Upili (Secondary), Ambapo Alihudumu Kama Waziri wa Afya na Chakula.
Mnamo Mwaka 2019, Alifanikiwa Kuchaguliwa Kuwa Mjumbe wa Kamati Ya Utekelezaji wa Kata ya Kivule, Kwenye Jumuiya Ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Na Kuhudumu Kwa Miaka Mitatu, Kwa Juhudi, Ubunifu, na Kujitolea.
Mnamo Mwaka 2020, Alifanikiwa Kuwa Mtia Nia Wa Nafasi Ya Ubunge wa Jimbo La Ukonga, Akichuana Na Wanasiasa Wakongwe, Lakini Hakushinda
Mnamo Mwaka 2022, Alifanikiwa Kugombea Kwenye Nafasi Ya Ukatibu wa Seneti - Mkoa wa Dar Es Salaam, Lakini Hakushinda
Baadaye Mwaka Huo (2022), Akagombea Nafasi Ya Ujumbe wa Mkoa Kutokea Kata ya Kivule Kupitia Jumuiya Ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Na Alifanikiwa Kushinda Na Kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Mkoa Kutokea Kata Ya Kivule, Akifanya Kazi Zake Kwa Bidii Na Kujitolea, Na Alihudumu Kwa Muda Mfupi, Kisha Kuchukua Fomu Ya Ugombea wa Nafasi Ya Uwenyekiti wa Wilaya Ya Ilala, Kupitia Jumuiya Ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Na Kupendekezwa Kugombea Nafasi Ya Ujumbe wa Mkoa wa Wilaya ya Ilala Kupitia Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ambapo Alifanikiwa Kuchaguliwa Kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Mkoa Kwenye Wilaya Ya Ilala, Mkoa wa Dar Es Salaam, Nafasi Anayoihudumu Mpaka Sasa.
NDOTO ZAKE
Kuwatumikia Watanzania Na Kuwa Sehemu Ya Kutatua Changamoto Zinazoikabili Taifa Lake
Kwasasa Anajishugulisha Na Kampeni Ya Kupandisha Ufaulu Kwenye Shule Za Kata, Ambapo Amefanikiwa Kutembelea Shule Kadhaa za Kata, Ili Kujua Changamoto, Na Kuweza Kujadili na Kuja Na Mbinu Zitazowasaidia Walimu Kuchochea Ufaulu Kwenye Shule Hizo.
Hii Ni Katika Kupambana Na Adui Ujinga.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI
Ni Mfanyakazi Kwenye Kampuni ya Majiko, Inayohusisha Kuuza na Kusambaza Majiko Ya Nishati Safi Ya Kupikia, Kwenye Taasisi Mbalimbali Kama Shule, Hoteli, Na Kadhalika.
MAHUSIANO
Janeth Thomson Mwambije Hajaolewa, Pia Hakuwahi Kuolewa Hapo Kabla
MAPENDELEO
Anapenda Kusikiliza Muziki, Kuogelea, Na Kusafiri Sehemu Mbalimbali.