TANGAZO

TANGAZO

MKURUGENZI WA TANESCO AFARIKI DUNIA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Aprili 13, 2025 katika ajali iliyotokea wilayani Bunda mkoani Mara.


Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evans Mtambi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amefafanua kuwa limetokea kati ya saa 6 hadi 7 usiku wa kuamkia leo.


"Ni kweli tukio lipo na amefariki dunia ila wasiliana na RPC atakuwa na taarifa kwa kina," amesema Mtambi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kutoa taarifa baadaye kidogo.


"Ndio nimefika eneo la tukio naomba muwe na subira nitakupa taarifa baadaye," amesema Kamanda Lutumo.


Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mara, Nickson Babu amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda huku wakisubiri taarifa zaidi kuhusu taratibu nyingine.

Chanzo - Matukio Daima Media

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com