TANGAZO

TANGAZO

PPRA YAWAJENGEA UWEZO WALEMAVU WASIOONA

 


Mamlaka ya udhibiti na ununuzi wa Umma (PPRA) Leo April 25,2025 imetoa mafunzo maalumu kwa Walemavu Wasioona  juu ya upendeleo kwa makundi maalum katika ununuzi wa Umma.


Mafunzo hayo yametolewa kwa Wanachama wa Jumuiya ya Wasioona Tanzania na Chama cha wasioona Tanzania ambayo yamelenga  kuelimisha makundi  hayo juu ya haki zao na fursa ambazo wanaweza kuzitumia katika mchakato wa ununuzi wa umma.


Akifungua mafunzo hayo mapema leo Aprili 25,2025 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Dennis  Simba amesema lengo la mafunzo  hayo ni kuhakikisha makundi  hayo yanapata fursa za kibiashara na kuchagia ukuaji wa uchumi wa nchi.


Amesema Jukumu la PPRA ni kuhakikisha kuwa mifumo ya ununuzi inazingatia Misingi ya usawa, haki na uwazi .


"Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na juhudi kubwa za serikali za kuhakikisha kuwa makundi maalum ya yanapata upendeleo Katika ununuzi wa Umma hii ikiwa ni pamoja na kutoa,Sheria ya ununuzi ya 2023,pamoja na kanuni zake za mwaka 2024 zinatoka miongozo ya namna ambayo makundi maalum yanaweza kunufaika na upendeleo Katika mchakato wa ununuzi"amesema.


Akiyataja makundi hayo Simba amesema  ni wanawake,vijana,watu wenye Ulemavu na wazee huku aakibainisha kuwa  idadi ya vikundi maalum 280 vilivyokamulisha Usajili na uhuishaji wa taarifa zao Katika mfumo wa ununuzi wa Umma yaani NeST ambapo vikundi hivyo vimepata TUZO za mikataba zilizotolewa kwa makundi maalum .

"Jumla ya tuzo 440 zenye thamani ya shilingi Bilioni 15 Miongoni mwao vijana ni vikundi 163 sawa na asilimia 58,wanawake vikundi 96 sawa na asilimia 34,watu wenye mahitaji maalum (walemavu) ni vikundi 4 sawa na asilimia 2 na wazee vikundi 17 sawa na asilimia 6."amesema.


Aidha amesema kila mmoja ana Jukumu kuhakikisha anafaidika na fursa zilizotolewa kwa makundi maalum katika sekta ya ununuzi wa Umma.


"Mafunzo haya ni mwanzo mzuri wa safari ya kuelewa na kutumia haki hizi kuboresha mazingira ya biashara na kuongeza tija Katika uchumi wa nchi yake"alisisitiza.


Kwa Upande Mratibu wa Wanawake na Watoto kutoka Chama cha Wasioona Tanzania Dorice Kulanga na ameishukuru PPRA  kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yamewasaidia kupata elimu juu ya namna ya kuchagamkia fursa mbalimbali  zitokanazo na tenda za Serikali. 


Aidha ameiomba Serikali  kuweka vigezo rafiki kwao au Masharti nafuu katika utoaji wa tenda ili waweze kupata hizo tenda.



Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com