Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema amepokea kwa unyenyekevu na shukrani ujumbe wa hayati Papa Franci aliouandika kwa ajili yake, kwa nchi yetu na kwa Watanzania wote siku chache kabla ya kuaga dunia.
Hii ndio Ujumbe wa Papa Francis Kwa Watanzania.👇
Rais samia kupitia ukurasa wake wa Instagram Kupitia ujumbe wake kwa umma, Rais Samia amesema:
"Kwa unyenyekevu na shukrani, nimepokea ujumbe wa hayati Papa Francisko kwangu, kwa nchi yetu na kwa Watanzania wote, aliouandika siku chache kabla Mwenyezi Mungu hajamwita kwake, na kumkabidhi Balozi wa Vatican hapa nchini, Askofu Mkuu Angelo Accattino. Tuendelee kumwombea kwa Mwenyezi Mungu alale mahali pema."