TANGAZO

TANGAZO

WAFUGAJI WATAKIWA KUTOJICHUKULIA SHERIA MKONONI

 


Polisi Kata ya Mbuyuni Wilaya ya Songwe Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Magdalena Ntandu Aprili 22, 2025 amewataka wafugaji wa kata hiyo kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi ambayo ni kosa kisheria.


"Acheni kujichukulia sheria mkononi pindi muwakamatapo wahalifu wa mifugo yenu na badala yake wawafikishe kwenye vyombo vya sheria ili wachukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani" alisema Mkaguzi Magdalena.


Vilevile, Mkaguzi Magdalena aliwataka wafugaji hao kudhibiti mifugo ya kwenda kwenye mashamba ili kuepusha migogoro na wakulima.

Mkaguzi Magdalena alitoa wito kwa wafugaji hao kufanya shughuli za ufugaji katika maeneo tengwa ikiwa ni pamoja na kuchimba visima kwa ajili ya kunyweshea mifugo yao pamoja na kujenga mazizi salama na imara.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com