TANGAZO

TANGAZO

WASIRA AMJIBU MFUASI WA CHADEMA ALIYEOMBA CCM, SERIKALI KUMSAMEHE LISSU

 



-Amwambia Chama, Rais Samia wanaamini katika maridhiano, kutii sheria


-Asisitiza CCM haina visasi wala chuki na yeyote


-Amwambia Lissu anatuhumiwa kuikosea Jamhuri sio CCM, hivyo watamalizana mahakamani



Na Mwandishi Wetu


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira amewahakikishia Watanzania kwamba Chama hakina chuki wala kısası na mtu yeyote na kinaamini katika sera ya maridhiano.

Pia, amesema kuwa menyekiti au makamu mwenyekiti wa chama cha siasa haikupi uhalali wa kuwa juu ya sheria, hivyo iwapo utafanya kosa lolote Jeshi la Polisi litakukamata na sheria itachukua mkondo wake bila kujali nafasi uliyonayo.



Wasira alitoa kauli hiyo jana akiwa katika mkutano wa hadhara alipokuwa akizungumza na wana CCM na wananchi wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora ambako anaendelea na ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani, kuzungumza na viongozi wa CCM na kusikiliza kero za wananchi.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com