TANGAZO

TANGAZO

DKT. NCHEMBA ATOA WITO WA KUIMARISHA UTENGAMANO WA KIKANDA EAC



Na. Benny Mwaipaja, WF, Arusha

Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaosimamia masuala ya Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki, limekubaliana kusoma Bajeti Kuu za Serikali za nchi wanachama wa Jumuiya hiyo tarehe 12 Juni, 2025.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika huo wa 17 wa Baraza hilo uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Jijini Arusha. 


Alisema kuwa Baraza hilo pia limebuni kauli mbiu moja ya bajeti ya nchi za Afrika Mashariki ambayo inaonesha mwelekeo wa kibajeti itakayosomwa wakati wa uwasilishaji wa Bajeti baada ya kupita katika hatua nyingine kwa kuwa kwa sasa bado kaulimbiu hiyo ni mapendekezo.


Dkt. Nchemba alisema kuwa mkutano umepokea wasilisho la nchi wanachama kuhusu mwenendo wa viashiria vya uchumi jumla, hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa vigezo vya uchumi jumla vya mtangamano wa kikanda na vipaumbele vya bajeti kwa mwaka 2025/26 kutoka kwa nchi wanachama, 


Dkt. Nchemba alisema kuwa katika mkutano huo wamejadili taarifa ya mashauriano ya kibajeti kuhusu viwango vya pamoja vya Ushuru wa Forodha vya Afrika Mashariki kwa mwaka 2025/26.

Aidha, Dkt. Nche,mba alisema kuwa Mawaziri hao wa Fedha wamekubaliana utaratibu wa uendeshaji wa jumuiya ikiwemo utoaji fedha za uendeshaji wa Jumuiya ambayo ni maelekezo ya Wakuu wa nchi katika Kikao kilichopita, lakini pia kukamilisha utaratibu wa taasisi ya fedha ambao mchakato wake ulifanyika katika vikao vilivyopita ambao unasubiri hatua za mwisho ili uende katika hatua za utekelezaji.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, Bw. Yusuf Mwenda, Viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com