TANGAZO

TANGAZO

HARMONIZE NA SARAH KIROHO SAFI TU!

 


Ndivyo tunavyoweza kusema kwa kile kinachoonekana sasa, licha ya kuachana kwao kwa muda mrefu kwa kile kilichodaiwa ni Harmonize alizaa nje ya ndoa yao, ni wazi hakuna aliyeondoka na kinyongo dhidi ya mwenzake.

Mwimbaji wa Bongo Fleva, Harmonize na mke wake, Sarah Michelotti kutoka nchini Italia walifunga ndoa kwa siri iliyohudhuriwa na watu wachache Septemba 2018 jijini Dar es Salaam.

Walikuja kuachana Desemba 2019 baada ya Sarah kumshutuma Harmonize kuzaa nje ya ndoa na Konde Boy alikiri hilo ni kweli na kusema ni vigumu kuikana damu yake.

Harmonize alianzisha mahusiano na Sarah baada ya kuachana na Jacqueline Wolper ambaye ndiye mpenzi wake wa kwanza na maarufu kumuweka wazi kwa mashabiki wake na kujiachia vilivyo kwenye mitandao ya kijamii.

Ingawa Harmonize na Sarah ameachana hakuna hata mmoja aliyefuta picha za mwenzake kwenye ukurasa wake wa Instagram, hii ni tofauti na watu wengi maarufu ambapo baada ya kuachana huvuta picha zote, huku wengine wakienda mbali hadi kufuta tattoo walizochora kipindi penzi limekolea.


Hadi sasa ukienda kwenye ukurasa wa Instagram wa Sarah hajafuata picha hata moja ya Harmonize, bado zipo hadi matangazo yake na promosheni ya nyimbo zake. Hivyo Hivyo kwa Harmonize, hajafuta picha yoyote ya Bibie toka wamenza mapenzi yao mwaka 2017 baada ya Konde Boy kuachana na Jacqueline Wolper.



Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com