TANGAZO

TANGAZO

MAKALA: WANAUME NDANI YA NDOA KULEA WATOTO WASIOKUWA WAKWAO: MOTO MKUBWA UNAO WAKA NDANI YA FAMILIA ZA KISASA

 


Katika zama hizi za maendeleo ya teknolojia na mitandao ya kijamii, tumeshuhudia mambo mengi yakifichuliwa hadharani – mengine yakiwa ya kushangaza, mengine ya kuumiza. Lakini kati ya yote, ushuhuda wa wanawake wanatoa siri kwa kuzaa nje ya ndoa na kuwa waume zao wanalea watoto wasiowazaa bila wanaume hao kujua ukweli wa kinacho endelea, na shuhuda hizo zimekuwa miongoni mwa mada nzito zinazoleta simanzi, hasira na taharuki kubwa katika jamii ya sasa.

Kupitia akaunti za siri kama zile za Instagram confession pages, WhatsApp groups na Facebook anonymous platforms, wanandoa – hasa wanawake – wamekuwa wakifunguka kuhusu maisha yao ya ndoa. Simulizi nyingi zinaonesha jinsi baadhi yao walivyopata ujauzito nje ya ndoa, kisha wakaamua kuficha ukweli huo na kuleta mtoto ndani ya ndoa wakijua kabisa si wa mume aliyepo.

Chanzo cha tatizo kutokana na melezo ya shuhuda hizo nyingi kutoka wa wahusika inaonyesha dhahiri:-

Udhaifu wa maadili: Maisha ya "mimi kwanza" yamepoteza misingi ya uaminifu na heshima kwa taasisi ya ndoa.

Shinikizo la ndoa kwa haraka: Wengine huingia kwenye ndoa wakiwa tayari na ujauzito au watoto wa nje kwa hofu ya aibu au kutaka "kuhalalisha" maisha.

Ukosefu wa mawasiliano: Wanandoa wengi hawazungumzii kwa uwazi masuala nyeti, jambo linaloleta migogoro na uongo.

Mitindo ya maisha ya kisasa: Safari za kikazi, uhuru mkubwa wa kifedha, na mawasiliano ya kimtandao yameongeza nafasi ya usaliti.

Athari Zake Ni Kubwa Kuliko Tunavyodhani


1. Ndoa Kuvunjika kwa muda mfupi na kwa wingi: Ripoti za RITA zinaonesha ongezeko la talaka kutoka 10,150 (2022) hadi 12,000 (2023) – wengi wakieleza sababu ni ukosefu wa uaminifu na ugunduzi wa watoto wasio wa ndoa.

2. Kuongezeka kwa Magonjwa ya Zinaa: Kutokuwa waaminifu kunahatarisha afya ya wanandoa. WHO imeripoti Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha maambukizi ya magonjwa ya zinaa, hususan kwa watu walio kwenye mahusiano ya muda mrefu.

3. Single Mothers na Watoto wa Kiume Waliochanganyikiwa: Kuongezeka kwa wanawake wanaolea watoto peke yao kunaleta changamoto za malezi ya upande mmoja. Watoto hawa hukua bila muundo wa baba na mama, hali inayoweza kuathiri maendeleo yao ya kihisia, kitabia na hata kimaadili.

4. Wanaume Waliojeruhiwa Kisaikolojia: Wanaume wengi wanagundua watoto si wao baada ya miaka mingi ya uwekezaji wa mapenzi, fedha na muda. Wengine huingia kwenye msongo wa mawazo, hasira, au hata mauaji.

5. Vijana Wanaoogopa Ndoa: Wimbi la simulizi hizi limefanya vijana wengi kuiona ndoa kama "hatari ya kihisia" badala ya baraka ya maisha. Hili linaweka hatari ya jamii kukosa familia imara za baadae.

Sauti Kutoka Kwa Wataalamu:

Mchungaji Joseph Mwinuka wa kanisa moja jijini Dar es Salaam anasema:

“Uongo wa uzazi ni laana inayojirudia. Mwanamke anapombambikizia mume mtoto, si tu anamuumiza, bali anavuruga roho ya familia nzima. Tunahitaji kurudi kwenye maadili ya hofu ya Mungu.”

Bi. Clara Nyarandu, mshauri wa ndoa na familia:

 “Wanawake wanafanya hivi kwa sababu ya hofu ya kuachwa, lakini matokeo yake ni mabaya zaidi. Kila mtu anastahili kujua ukweli juu ya mtoto wake – kwa afya ya akili, heshima na haki ya msingi.”


Ushauri kwa Jamii Nzima


Kwa Wanawake: Ukimpachika mwanaume mtoto asiye wake bila kumwambia, unamnyima haki yake ya msingi na unavunja msingi wa uaminifu.Na kuzaa nje ya ndoa hakufuti maumivu au historia ya makosa aliyowahi kukukosea huyo mume wako, bali unapandikiza chuki na mizizi ya msumari wa moto usio zimika kwa urahisi.na kutoa shuhuda kwenye mitandao kwa siri hakufuti ukweli, usio futika– tafuta msaada wa kitaalamu, tafakari upya na sema ukweli kwa hekima, mana hakuna siri chini ya jua na kuna msemo usema “every secret has its way of coming out’ Tafakari

Kwa Wanaume: Jaribuni kupita njia zilizo sahihi wakati wa uchumba wenu na baada ya kuingia kweye ndoa, matendo yenu kwa wake zetu labda ni kabla au baada ya ndoa hupelekea wanawake hawa kuishi na vinyongo na hasira nyingi bila wewe kujua na kuoelekea kuchukua maamuzi yatakayo kuumiza maisha yako yote. Siyo kila mtoto anayefanana au kutofanana na wewe ni lazima awe si wako.

Kwa Wazazi na Viongozi wa Dini: Tukaze msumari kwenye mafunzo ya maadili, maandalizi ya ndoa, na kuhimiza vijana kuchagua wenza kwa uangalifu, si kwa shinikizo. Na kuwaaminisha vijana katika imani ya uvumilivu na utulivu.

Kwa Serikali na Asasi za Kiraia: Kuwe na kampeni maalum za maadili ya familia, elimu ya uzazi, na malezi bora ili kuzuia kizazi kijacho kurudia makosa haya.

Inaendelea.......

Imeandikwa Na. Sharon Chamwingi Mpondachuma




Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com