TANGAZO

TANGAZO

MAAFISA FORODHA WA NCHI NANE WAPEWA MAFUNZO ARUSHA


Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Fainahappy Kimambo akifungua Mkutano wa pamoja wa Maafisa wanaosimamia utekelezaji wa Itifaki ya Montreal inayohusu udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni na Maafisa Forodha wa Nchi nane za Afrika unaofanyika jijini Arusha leo tarehe 7 Mei, 2025.



Mwakilishi kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa Bw. Patrick Salifu akitoa neno la ukaribisho wakati wa Mkutano wa pamoja wa Maafisa wanaosimamia utekelezaji wa Itifaki ya Montreal inayohusu udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni na Maafisa Forodha wa Nchi nane za Afrika unaofanyika jijini Arusha leo tarehe 7 Mei, 2025.


Maafisa forodha wametakiwa kubainisha changamoto zilizopo katika biashara na usafirishaji wa kemikali na kujengeana uwezo wa namna ya kuzitatua.

Afisa Mazingira Mkuu kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Fainahappy Kimambo ametoa wito huo fungua Mkutano wa pamoja wa Maafisa wanaosimamia utekelezaji wa Itifaki ya Montreal inayohusu udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni na Maafisa Forodha wa Nchi nane za Afrika unaofanyika jijini Arusha leo tarehe 7 Mei, 2025.

Amewataka maafisa hao kuendelea kusimamia na kudhibiti biashara na usafirishaji wa chemicali zinazomongonyoa tabaka la ozoni kikamilifu na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi na nchi katika kusimamia na kudhibiti usafirishaji na biashara haramu ya kemikali zinazomong’onyoa tabaka hilo.

Aidha, Bi. Kimambo amesema Nchi Wanachama wa Itifaki ya Montreal zina wajibu wa kuendelea kuunga mkono tafiti zinazofanyika ili kuhakikisha ulinzi wa tabaka la ozoni kwani shughuli hizi zitatoa mwongozo wa kutuwezesha kupata mafanikio zaidi katika miaka ijayo.

Amesema Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo itaendelea kuwajengea uwezo Maafisa forodha ili kuwawezesha kudhibiti uingizaji nchini mwao wa kemikali zinazodhibitiwa chini ya Itifaki.

Vilevile, amehimiza Mfuko wa Kimataifa wa Utekelezaji wa Itifaki ya Montreal kuendelea kutoa fedha ili kusaidia Taasisi zetu kutekeleza matakwa ya Itifaki.

Ameongeza kuwa lengo ni kuimarisha ushirikiano baina ya maafisa forodha na wasimamizi wa utekelezaji wa Itifaki ya Montreal katika udhibiti wa uingizaji wa kemikali na vifaa vinavyodhibitiwa chini ya Itifaki hii katika mipaka ya nchi.

Alisema pia, katika mkutano huo washiriki watapata fursa ya kutambua changamoto zilizopo katika biashara na usafirishaji wa kemikali na namna ya kuzitatua.

Bi. Kimambo aliongeza kwa kusema kuwa mafunzo hayo yamewakutanisha maafisa forodha na wasimamizi wa Itifaki ya Montreal wapya kuhusu matakwa ya Itifaki ya Montreal.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Bw. Patrick Salifu alisema kukua kwa biashara haramu katika bidhaa zote zinazodhibitiwa zikiwemo majokofu yanayohitaji kudhibitiwa.

Kuna haja ya kuendelea kuwasiliana na mashirika ya forodha ili kujumuisha Itifaki ya Montreal inayohusiana na shughuli zao, kama vile kutatua changamoto hizo.

Sanjari na hilo pia, Bw. Patrick alitoa wito kwa vyuo vya mafunzo ya forodha kuhimizwa katika kutoa mafunzo maalumu ya Itifaki ya Montreal katika mitaala yao rasmi.

Aliongeza kuwa juhudi za pamoja zikiwemo mazungumzo, ushirikiano na madalali, wafanyabiashara na wasafirishaji, uratibu wa shughuli za forodha, na kuongeza ufahamu ni muhimu za kusaidia kupambana na biashara haramu. 

Mkutano huo wa siku tatu umehudhuriwa na Wawakilishi kutoka Shirika la Forodha Duniani (WCO), Shirika la Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira (UN Environment); Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC), Maafisa wanaosimamia utekelezaji wa Itifaki ya Montreal na forodha kutoka nchi za Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda na mwakilishi kutoka Wakala wa Elimu ya Mafunzo ya Uvuvi.








Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com