TANGAZO

TANGAZO

RAIS SAMIA AMLILIA CHARLES HILARY

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa amepokea kwa masikitiko kifo cha Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar, Charles Hilary  kilichotokea leo Mei 11, 2025

Rais Samia kupitia Ukurasa wake wa Instagram ameandika hivi "Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Charles Hilary, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar kilichotokea leo Mei 11, 2025."

"Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, familia, ndugu, jamaa na marafiki na wadau wote wa sekta ya habari nchini kwa msiba huu," ameandika Rais Samia.

"Ndugu Charles Hilary atakumbukwa kwa mchango wake adhimu wa zaidi ya miaka 40 katika kukuza sekta ya habari nchini tangu akiwa redioni hadi kwenye televisheni, pamoja na unasihi kwa wanahabari wachanga."


Namuomba Mwenyezi Mungu aijaalie familia yake uvumilivu na subra katika kipindi hiki kigumu, na ailaze roho ya mpendwa wetu mahala pema.


Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com