TANGAZO

TANGAZO

SERIKALI YATOA KIPAUMBELE KUDHIBITI WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU

 


Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kudhibiti changamoto ya Wanyamapori wakali na waharibifu na kuhakikisha takwimu za vifo na majeruhi zinapungua au kutokuwepo kabisa.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) ameyasema hayo Mei 19,2025 alipokuwa akihitimisha Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii Bungeni jijini Dodoma.


"Wakati umefika wa kulinda maeneo ya hifadhi kwa njia ya teknolojia hii ni pamoja na kufunga kola maalum kuona tembo wanatoka na kununua ndege nyuki (drones)" amesema Mhe. Chana.


Ameongeza kuwa Serikali itanunua helikopta mbili, itajenga vizimba kudhibiti mamba na viboko, itachimba mabwawa kuhakikisha maeneo ya hifadhi yana maji ya kutosha na kununua vitendea kazi vya pikipiki na magari kusaidia Askari Uhifadhi.


Aidha, Mhe. Chana amefafanua kuwa pia Serikali itaendeleza ujenzi wa vituo vya Askari, itanunua mabomu baridi na kutoa mafunzo ya wanyamapori kwa Askari wa Vijiji (Village Game Scouts) ili kusaidia vijana kuhakikisha wanaweza kudhibiti wanyamapori.


"Changamoto ya tembo ,nyani ,mamba kiboko tunaenda kushughulikia na kuweka mkakati wa kukabiliana nao" amesisitiza Mhe. Chana.



Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com