Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo, tarehe 13 Mei 2025, ameshiriki ibada maalum ya mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Cleopa David Msuya.
Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa la KKKT Kristo Mchungaji Mwema, Dayosisi ya Mwanga, Jimbo la Kaskazini, Usharika wa Usangi Kivindu, mkoani Kilimanjaro.






