TANGAZO

TANGAZO

TOENI TAARIFA MAPEMA WIZARANI - NAIBU WAZIRI KITANDULA

 


Na. Anangisye Mwateba-Bungeni Dodoma

Maafisa wanyamapori wa Halmshauri za wilaya wametakiwa kutoa taarifa za uharibifu unaofanywa na wanyamapori kwa haraka Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuweza kufanya malipo ya kifuta jasho na machozi kwa mali zilizoharibiwa au vifo vilivyosababishwa na changamoto ya wanyama wakali na waharibifu.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula alipokuwa akijibu swali la Mhe. Mohamed Lujuo Monni aliyetaka kujua Serikali itatatua lini changamoto ya uvamizi wa Tembo mashamba ya Vijiji vinavyopakana na Pori la akiba la Swagaswaga Wilaya ya Chemba – Magungu

Aidha  Kitandula alisema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) imekamilisha kuchimba bwawa lenye ujazo wa lita 20,750,000 za maji katika Pori la Akiba Swagaswaga ili kuwezesha wanyamapori kupata maji ndani ya hifadhi na kupunguza uwezekano wa wanyamapori kwenda kutafuta maji katika maeneo ya wananchi.

Serikali inaendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia ikiwemo ndege nyuki (Drone) na mabomu baridi katika kukabiliana na changamoto ya Tembo kwenye eneo hilo.

Vilevile TAWA inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kufanya doria za mwitikio wa haraka. Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, jumla ya matukio 15 yaliripotiwa ambapo doria zenye siku 123 zimefanyika katika maeneo yanayopakana na Pori hilo ikiwemo Kijiji cha Magungu Wilaya ya Chemba.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com