TANGAZO

TANGAZO

WAZIRI MASAUNI AELEZA MKAKATI UTEKELEZAJI PROGRAMU MABADILIKO YA TABIANCHI ‎


Na mwandishi wetu

‎Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Masauni amefanya mkutano wa kimkakati wa uwili (Bilateral Meeting) kati ya Tanzania na Viongozi wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya ( Europian Union) . Katika Mkutano huo Waziri Masauni ameelezea mkakati wa Tanzania katika utekelezaji wa programu za Mabadiliko ya Tabianchini. 



Mkutano wa Majadiliano hayo umefanyika Mei 7 2025 ,pembezoni mwa Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira Duniani unaoendelea jijini Copenhagen, Denmark.


‎Mkutano huo umehudhiriwa na viongozi wakuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya  akiwepo Bw. Wopke HOEKSTRA  Kamishna wa  Mazingira wa Ulaya,  Bw. Krzysztof Bolesta, ambaye ni Katibu wa Nchi Wizara ya Hali ya Hewa na Mazingira- Poland. Bw. Bolesta amemwakilisha Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya ambapo kwa sasa nchi ya Polend ndio  mwenyekiti wa EU. Aidha viongozi hao waliambatana  na  Bw. Christian Stenberg, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mazingira, Nishati na Fedha wa Denmark. Denmark inatarajiwa kuchukua uenyekiti wa EU mara ifikapo Julai mwaka huu.


Katika Mkutano huo Waziri Masauni ameambatana na  Mshauri wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu masuala ya Mazingira na mabadiliko ya Tabianchi Dkt. Richard Muyungi, Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden pamoja na wataalam kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

‎Pamoja na masuala ya kubadilishana mawazo kuhusu vipaumbele kabla ya vikao vya Bonn na COP30, na Mwelekeo wa Nchi za kiafrika ambapo Tanzania ni mwenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika ( AGN). Waziri Masauni alieleza kuhusu vipaumbele vitatu vya Tanzania ambavyo ni kuendelea kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia njia mbalimbali vikiwamo vitu vya asili; kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa watanzania kutumia nishati safi ya kupikia hadi kufikia kiwango cha asilimia 80 ifikapo mwaka 2034

‎na kuendelea kuzijengea uwezo Taasisi zinazoratibu masuala ya biashara ya kaboni nchini.

‎Waziri Masauni amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Umoja huo wa Ulaya kuangalia namna bora ya kuiwezesha katika masuala ya kujengea uwezo, misaada ya kifedha yenye masharti nafuu, ruzuku na Teknolojia ya upimaji wa kiwango cha kaboni.

‎Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Sasa wa EU, Bw. Krzysztof Bolesta, ameipongeza Tanzania kwa namna ilivyochukua hatua za kuanzisha Kituo cha Kaboni ambacho ni cha  mfano kwa nchi za Afrika. Aidha, alieleza kuwa siku zote Umoja wa Ulaya umekuwa ukifanya kazi na kuongoza kwa mfano mzuri na kwa kudumisha uwazi na haki na hivyo itaendelea kuhakikisha inatenda haki ya kutimiza ahadi  zake zote za ufadhili wa programu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchini. 

‎Aidha Bw. Bolesta alimalizia kwa  kuahidi kuendelea kushirkiana na Tanzania katika makabiliano ya mabadiliko ya Tabianchi.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com