Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa shirikisho la Makampuni ya Italia (FEDERISPARMIO) wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo Guido Mucelli, Mazungumzo yaliyofanyika Jijini Roma nchini Italia leo tarehe 23 Juni 2025.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha zaidi ushirikiano wa ubia baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni mbalimbali zilizo chini ya shirikisho hilo kufanya uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za kimkakati.