Wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria leo Juni 11, 2025 wamekutana na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Albert Chalamila.
Pamoja na mambo mengine Wataalamu hao wamekuja na ujumbe maalum wa Kampeni Kabambe ya Mama Samia Legal Aid ambayo inatarajiwa kuzinduliwa katika Mkoa huo hivi karibuni.




