Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Daniel Godfrey Chongolo kuwania ubunge wa Jimbo la Makambako,ikiwa ni uteuzi wa awali wa watakaoshiriki zoezi la kura za maoni.
Chongolo atachuana na aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo Ndugu Deo Kasenyanda Sanga.
Katibu wa NEC Itikadi,Uenezi na Mafunzo,CPA Amos Makalla ametangaza majina hayo leo Julai 29, 2025 alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Ofisi za chama hicho jijini Dodoma.