Wachimbaji wadogowadogo wa Madini wa Kijiji cha Matanda Kata ya Mbangala Wilaya na Mkoa wa Songwe wametakiwa kuzingatia suala la usalama katika shughuli zao za uchimbaji ikiwa ni pamoja na changamoto wanazokumbana nazo ni pamoja na kutokuwa na vifaa vya kinga, kutokujua mbinu bora za uchimbaji salama, na ukosefu wa elimu juu ya athari za kiafya zinazoweza kuwapata kutokana na mazingira hatarishi ya kazi hiyo.
Rai hiyo ilitolewa Julai 21, 2025 na Polisi kata ya Mbangala Mkaguzi wa Polisi Peter Selemani na kuwaeleza “hakuna kazi bora zaidi ya usalama wako" alisema kuwa si msemo tu, bali ni wito ambao unamtaka kila mchimbaji mdogo wa madini kujitoa katika hatari kwa sababu ya kipato. Uhai na afya ni rasilimali ya msingi ambayo haipaswi kuwekwa rehani.
Mkaguzi Selemani, aliwataka wachimbaji hao Kutumia vifaa vya kujikinga kama helmeti, viatu maalum, glovu na maski Kufuata taratibu na kanuni za uchimbaji salama ikiwa ni pamoja na Kushirikiana na mamlaka husika ili kupata mafunzo ya mara kwa mara kuhusu usalama kazini ili waepukane na ajali zinazoweza kuepukika.
Kwa Upande wao wachimbaji hao, kutokana na elimu hiyo watafanya kazi katika mazingira yanayozingatia usalama wao. Hatuwezi kuendelea kuchimba bila vifaa kinga, kwani tunahatarisha maisha yetu kwa kuwa tasnia ya wachimbaji wadogo wa madini katika kata ya Mbangala inaweza kuwa mfano wa kuigwa kwa uwajibikaji na ulinzi wa rasilimali watu na kufanya kupata maendeleo endelevu ya kila mchimbaji na kuwa na usalama mahala pa kazi muda wote.