TANGAZO

TANGAZO

MADEREVA WA POLISI WASISITIZWA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA KULINDA UHAI WA WENGINE


Madereva wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe wametakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali na kulinda usalama wa watumiaji wengine wa barabara.


Hayo yamesemwa Julai 03, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga alipofanya kikao na madereva hao katika ukumbi wa Polisi Vwawa Wilaya ya Mbozi Mkoani humo ambapo alisisitiza ukaguzi wa magari ya serikali kabla na baada ya safari ili kuendelea kujihakikishia usalama wa kutekeleza majukumu ya kila siku bila ajali.


"Niwatake kuhudhuria katika vyuo vya ufundi vinavyotambulika na serikali ili kujiongezea ujuzi zaidi katika kuvijua vyombo vya moto pamoja na sheria, kanuni, alama na michoro ya barabarani ili kuepuka ajali zinazosababishwa na uzembe.


Kwa upande wake, Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban alisema dereva mzuri anatakiwa kuwa na ujuzi na ufahamu wa chombo cha moto anachokiendesha ili aweze kubaini changamoto itakayojitokeza na kuweza kuitolea taarifa kwa ajili ya matengenezo kitendo kitachopelekea vyombo vya moto vya serikali kutumika kwa muda mrefu vikiwa imara muda wote.


Naye, Mkuu wa Usimamizi wa Magari ya Polisi Mkoa wa Songwe Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Kesbert Kapondo amesema pamoja na madereva hao kujituma katika majukumu wanayopangiwa wanatakiwa kuwa na udereva wa kujihami pindi inapolazimika kuliko kulazimisha kuendesha gari kwenye maeneo hatarishi kitendo ambacho kitapelekea uchakavu wa vyombo hivyo na kudumaza utoaji wa huduma kwa jamii jambo ambalo si sawa.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com