Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa siku moja wa Tume na asasi za kiraia kuhusu uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika leo Julai 30, 2025 Jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa siku moja wa Tume na asasi za kiraia kuhusu uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika leo Julai 30, 2025 Jijini Dar es
Salaam.
Sehemu ya wajumbe wa management ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ikiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya washiriki kutoka asasi za kiraia wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Baadhi ya washiriki kutoka asasi za kiraia wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume
Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Kailima Ramadhani akizungumza wakati wa Mkutano
wa siku moja wa Tume na asasi za kiraia kuhusu uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Mkutano huo umefanyika leo Julai 30, 2025 Jijini Dar es Salaam.
***************
Na. Mwandishi Wetu Taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu zimetakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanunina maelekezo ya Tume. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele wakati akifungua
mkutano wa Tumena taasisi na asasi
hizoleo Julai 30, 2025 jijini Dar es
Salaam. ”Nitoe rai kwenu haswa wale
mliopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura kuzingatia sheria, kanuni na
maelekezo ya Tume wakati wote wa utekelezaji wa zoezi hilo la kutoa elimu ya
mpiga kura,” amesema Jaji Mwambegele. Amesisitiza kuwa katika kipindi cha uchaguzi Tume itafanya kazi kwa karibu
na taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura. ”Niwaombe msichoke kuwasisitiza na kuwahimiza
wadau na wananchi kwa ujumla kuzingatia Sheria za Uchaguzi, Kanuni na Maelekezo
ya Tume. Tume nayo kwa upande wake itaendelea kuzingatia Sheria za Uchaguzi na
Kanuni katika michakato yote ya uchaguzi,”amesema. Jaji Mwambegele ameongeza kuwa wakati wa kampeni uzoefu
unaonesha kuwa kunakuwa na joto la kisiasa linatokana na baadhi ya watu kukosa
uvumilivu wa kisiasa, hivyo ameziasa taasisi na asasi hizo kutumia nafasi yao
kuwaelimisha wananchi ili uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu. ”Kipindi hicho cha kampeni mnapaswa kuwahimiza
wananchi kupitia majukwaa yenu kuwa makini kwa kuhakikisha kuwa hawawi chanzo
cha kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu,” amesema. Kwa mujibu wa kifungu cha 10(1)(g)(h) na (i) cha
Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024, Tume inao wajibu
wa kutoa elimu ya mpiga kura nchini, kuratibu
na kusimamia taasisi na asasi zinazotoa elimu ya mpiga kura na kualika na
kusajili waangalizi wa uchaguzi. Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu Tume imetoa
kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura kwataasisi na asasi 164 kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura na taasisi na asasi 76 za ndani na 12 za kimataifa
zimepata kibali cha uangalizi wa uchaguzi. Baadhi ya wawakilishi wa taasisi na asasi hizo
wamesema wamejipanga rasmi kutoa elimu ya mpiga kura haswa kwa vijana wanaotarajia
kupiga kura kwa mara ya kwanza. Wamesisitiza kuwa watatoa elimu kwa mujibu wa sheria,
kanuni na maelekezo yaTume. Mwenyekiti wa Malezi Foundation Network, Mwalimu
Neema Kabale, amesema hatua hiyo
inalenga kuhakikisha kuwa vijana walioandikishwa kuwa wapiga kura kwa mara ya
kwanza wanapata uelewa wa kutosha kuhusu taratibu za kupiga kura.
Washiriki kutoka asasi za kiraia mbalimbali wakichangia hoja wakati wa majadiliano.
Washiriki kutoka asasi za kiraia mbalimbali wakichangia hoja wakati wa majadiliano.
Wakurugenzi kutoka Idara na Vitengo ndani ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakijibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa wakati wa majadiliano
Wakurugenzi kutoka Idara na Vitengo ndani ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakijibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa wakati wa majadiliano.
Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com