Kuelekea michuano ya CHAN 2024 inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mnamo Agosti 02, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Saalaam, Wafanyabiashara wa Jiji hilo wamesema wamejiandaa vizuri kuwahudumia wageni wa mashindano ya CHAN 2024 kwa kuonesha ukarimu wa Watanzania.
Kwa upande watoa huduma ya chakula wamesema wanafurahia ujio wa mashindano ya CHAN nchini sababu wana uhakika watanufaika katika biashara zao.
Akizungumza kuhusu maandalizi ya utoaji wa huduma hiyo Julai 29,2025 Mwenge Dar es Salaam, Mpishi wa Mgawa wa AFCON 2027 Bw. Hussein Omary alisema, amejipanga vizuri kuandaa vyakula mbalimbali vya Kitanzania na vya asili ya Afrika.
“Tunawakaribisha wageni wote wa CHAN kwenye mgahawa wetu ambao tayari tumeanza kuitangaza AFCON 2027, tumejiandaa vizuri kuwapatia huduma bora ya vyakula vya asili ya ya Kitanzania na Afrika,"alisema Hussein.
Michuani ya CHAN hapa nchini itachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na New Aman Zanzibar kwa kiingilio cha shilingi 10,000, VIP 5000 VIP B na C na mzunguko 2000.