TANGAZO

TANGAZO

DENI LA TAIFA NI HIMILIVU KWA VIPINDI VYOTE


Tathmini ya Uhimilivu wa Deni iliyofanyika Oktoba, 2024 ilionesha kuwa deni la Serikali ni himilivu katika kipindi cha muda wa kati na mrefu. Tathmini hiyo hufanyika kwa kuzingatia vigezo vya uhimilivu ambavyo ni uwiano wa deni halisi kwa Pato la Taifa; uwiano wa deni halisi kwa malipo ya nje; na uwiano wa malipo ya deni kwa mapato ya ndani na mapato yatokanayo na mauzo ya nje. 

Kwa mujibu wa Tathmini hiyo, viashiria vya deni la vilionesha kuwa mwaka 2024|25: 

Kwa mujibu wa Kitabu cha Hali ya Uchumi 2024, Uchambuzi wa deni la Taifa kwa mwaka 2024|25.

a) Deni la nje/GDP ni 24% Ukomo ni 40% Bado kuna nafasi ya 16. 

b) Deni la nje /Mauzo ya nje ni 123.8% Ukomo ni 180% Bado kuna nafasi 56.2%.

c) Deni la nje/Mapato ya nje ni 13.9% Ukomo ni 15% Bado kuna nafasi ya 1.1% 

d) Deni la nje/Mapato ya ndani ni 17.2% Ukomo ni 18% Bado tuna nafasi ya 0.8% 

e) Deni lote/Kwa Pato la Taifa (GDP) ni 40.4% Ukomo ni 55% Bado tuna nafasi 14.7%. 



 

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com