Jesca Magufuli ambaye ni Mtoto wa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, baada ya June 28, 2025 kuchukua rasmi fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Amewaomba kura kwenye Ukurasa wake wa Instagram.
Jesca ni Binti ambaye amejipambanua kama sauti ya matumaini kwa Vijana na Wanawake wa Tanzania akisimamia maadili, haki na maendeleo jumuishi ambapo amelenga kupeleka nguvu mpya ya kijana Bungeni, kusimamia ajenda za maendeleo kwa Vijana, Wanawake na Jamii kwa ujumla huku akihakikisha UVCCM inasikika, inaonekana na inawakilishwa kwa heshima katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hizi ni baadhi ya Comment za watu Mashuhuri na Wananchi baada ya kuomba kura kwa Wajumbe👇