Wakati Rais Samia Suluhu anaingia madarakani Wajasiliamali waliopewa mikopo binafsi (Personal loans ),thamani ya mikopo hiyo ilifikia jumla ya TZS 7Trilioni miaka minne baadae mikopo hii imefikia jumla ya TZS 14Trilioni sawa na ongezeko la TZS7Trilioni au 100% pia ni ongezeko la mara mbili.
Haya ni matokeo ya Uongozi wenye maono wa Rais Samia Suluhu Hassan unaotambua nafasi ya wajasilimali wadogo na wakati, ambao idadi yao ni 90% ya biashara zote duniani, wakichangia 50% ya ajira na karibu asilimia 70% ya uchumi wa dunia (Kitabu Cha Hali ya Uchumi 2024).