TANGAZO

TANGAZO

TANZANIA YATUMIA SH. BILIONI 330.2 KUNUNUA MABEHEWA 1,430

 


Chini ya Rais Samia, kupitia mradi wa Kwala Industrial Park, serikali imeunganisha eneo hili na reli ya kisasa ya SGR yenye urefu wa kilomita 18, hatua inayowezesha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kusafirishwa haraka na kwa ufanisi moja kwa moja hadi Kwala. 

Ili kuongeza uwezo wa usafirishaji, mabehewa 1,430 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 330.2 yameandaliwa, jambo linalopunguza utegemezi wa malori pekee, kupunguza gharama za usafirishaji na muda wa safari, na kuongeza usalama wa mizigo.

Kati ya mabehewa 1,430 mabehewa 264 yameshawasili kati yake 200 ni makasha (container carriers) na 64 ni ya mizigo isiyofungwa (loose cargoes).

Hatua hii inaiweka Tanzania katika nafasi bora ya kuimarisha biashara ya kikanda na kuongeza ushindani wa kiuchumi.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com