TANGAZO

TANGAZO

HATUA 15 KATIKA SIKU 100 ZA MUHULA WA PILI WA SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA KUTEKELEZA ILANI YA CCM YA 2025 - 2030

 




Tumefungua ukurasa mpya wa matumaini kwa taifa letu. Safari ya kutekeleza Dira 2050 imeanza. Azma ya Serikali nitakayoiunda pindi nitakapopata ridhaa yenu ni kuona mabadiliko yanayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Tutazingatia kazi na utu kwa kwa kila Mtanzania. Nikipata ridhaa ya wananchi kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025, katika siku 100 za uongozi wangu nitasimamia utekelezaji wa hatua zifuatazo kama sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM. 

1. Tutaanza rasmi kutekeleza sheria ya Bima ya Afya kwa Wote. Kwa kuanzia, ndani ya siku 100 tutazindua rasmi Mfumo wa Taifa wa Bima ya Afya kwa Wote kwa awamu ya majaribio, tukianzia kwa wazee, watoto, mama wajawazito na watu wenye ulemavu. Gharama za matibabu kwa makundi haya zitabebwa na Mfuko wa Taifa wa Bima. 

2. Serikali itaanza kugharamia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vya magonjwa yasiyoambukizwa, ikiwemo saratani, figo, moyo, sukari, mifupa na mishipa ya fahamu. Haya ndiyo magonjwa yenye gharama kubwa na ambayo wananchi wasio na uwezo wamekuwa wakishindwa kumudu gharama zake. 

3. Kuanzia sasa ninapoongea ni marufuku hospitali yoyote nchini kuzuia miili ya marehemu kuchukuliwa na ndugu zake hata kama gharama za matibabu za matibabu aliyopatiwa marehemu hajazilipwa. 



4. Serikali itaajiri wahudumu wa afya wapya 5,000, wakiwemo wauguzi na wakunga, ili kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.


5. Tutaanda mkakati madhubuti na ya kisanyansi kuhakikisha kila mtoto wa darasa la tatu anaweza kusoma, kuhesabu na kuandika bila shida.


6. Tutazindua mkataba (National Skills Compact) wa kitaifa wa ujuzi kwa viwanda mpango wa pamoja kati ya waajiri, vyuo vya ufundi stadi (TVETs) na vyuo vikuu kwa lengo la kulinganisha mafunzo na mahitaji ya sekta kipaumbele, kuanzia na nishati, TEHAMA, na viwanda vya kuongea thamani.


7. Tutaajiri walimu wapya 7,000 wa masomo ya hisabati na sayansi.


8. Nitazindua Mfuko wa Ajira kwa Vijana na Wanawake wenye wa thamani ya shilingi bilioni 200 ili kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya biashara ndogo na za kati na kuwezesha uendeshaji wa kampuni changa


9. Nitazindua programu maalum ya kurasimisha sekta isiyo rasmi kwa mama lishe, usafiri na usafirishaji na wajasiriamali wadogo.


10. Tutaanzisha programu maalum ya ujenzi wa mitaa ya viwanda kwa kila wilaya yenye kulenga kuzalisha ajira kwa watanzania kupitia kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, madini na misitu, pamoja na vifaa vya ujenzi.


11. Tutaanza utekelezaji wa Gridi ya Taifa ya Maji kwa lengo la kuwa na vyanzo vya uhakika vya maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, kilimo, mifugo na biashara. Gridi ya Taifa ya Maji itahusisha vyanzo vikubwa vya maji kutoka maziwa: Victoria, Tanganyika, na Nyasa, pamoja na mito mikubwa nchini.

12. Tutazindua miradi ya haraka ya nishati, ikiwemo umeme vijijini kwa kutumia nishati jadidifu (solar, wind), nishati safi ya kupikia. Hatua hii itapunguza utegemezi wa kuni na mkaa na kuhifadhi mazingira.

13. Kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na zege katika maeneo ya mijini na vijijini.

14. Tutaanzisha mfumo rafiki ya uwajibikaji ambapo mawaziri, wakuu wa mikoa na watendaji wengine wa serikali watatoa taarifa na kujibu maswali kutoka kwa wananchi kwa njia ya kidijitali na SMS bure.

15. Kuanzisha mazungumzo ya wadau wakiwemo asasi za kiraia, viongozi wa dini, wafanyabiashara na vyama vya siasa ya kuhuisha na kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya.


Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com