TANGAZO

TANGAZO

ZIARA YA MGOMBEA URAIS CCM : DKT. SAMIA AAHIDI KUENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA KILOSA - ULAYA- MIKUMI



Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara za kampeni za uchaguzi mkuu wa 2025 ambapo jana amefanya mikutano ya kampeni katika Wilaya ya Kilosa, ambapo amenadi sera zake kwa umati mkubwa uliomlaki katika wilaya hiyo. Dkt. Samia ameahidi kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara kwa kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kilosa–Ulaya–Mikumi, ambayo imeanza kujengwa na itakamilika ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo. 

Sambamba na hili, ameahidi kuwa endapo atachaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa Oktoba serikali yake itaendeleza ushoroba unaopita reli ya SGR kwa kujenga viwanda na maghala ili kuufanya kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji mpya. 

Huku akiwahimiza wananchi wa Kilosa kujitayarisha kwa fursa hizo zinazokuja kupitia uwekezaji wa kimkakati katika kipindi cha 2025-2030. Kuhusu changamoto za upatikanaji wa maji, Mhe. Dkt Samia ameahidi kuendeleza na kukamilisha miradi iliyokwisha kuanza sambamba na kuibua miradi mipya ya maji kwenye Wilaya ya Kilosa. 

Katika hatua nyingine Mgombea wa Urais na Mwenyekiti wa CCM Taifa ameahidi kumaliza migogoro ya ardhi kwa kuwa serikali yake itaipa kipaumbele sekta ya ardhi, Dkt Samia amesisitiza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake jumla ya hekari 53,475 za mashamba ambayo hayakuendelezwa yalifutwa , na hekari 21,872 zimepimwa na kugawiwa kwa matumizi ya kilimo, makazi na uwekezaji, ambapo Wananchi 8,557 kutoka vikundi 186 katika vijiji 11 wamenufaika na mgao huu. 

Dkt. Samia amesisitiza kuwa ugawaji utaendelea bila upendeleo, huku wale wenye uhitaji maalum wakipewa kipaumbele. 


Kuhusu Migogoro baina ya wakulima na wafugaji Dtk. Samia amesema kuwa imeanza kushughulikiwa kupitia programu ya Tutunzane, ambayo awali ilianza Mvomero na sasa inalengwa kuletwa Kilosa. 

Ameahidi kuwa serikali ya CCM endapo watapewa ridhaa na wananchi itaongeza maeneo ya malisho kutoka ekari milioni 3.46 ya sasa hadi ekari milioni 6 mwaka 2025-2030 ili kupunguza migogoro. 

Kuhusu kilimo, Mhe. Dkt. Samia ameeleza kuwa akipewa ridhaa na watanzania katika kipindi kingine ataendeleza sekta ya kilimo kwa kuendelea na mpango wa kutoa ruzuku za mbolea, mbegu na pembejeo kwa wakulima, sambamba na kukamilisha ujenzi wa Bwawa la Idete ili litumike kwa 

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com