Chini ya Rais Samia, mradi mkubwa wa maji wa Arusha ulioko Mkoa wa Arusha umejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 520 (takribani USD milioni 200). Mradi huu utanufaisha wananchi 850,000 moja kwa moja.
Mradi huu utazalisha maji lita milioni 200 kwa siku sawa na lita bilioni 73 kwa mwaka. Kukamilika kwa mradi huu kunalifanya Taifa kuwa na upatikanaji wa maji kwa asilimia 91.6 mjini na 83.0 vijijini.
Hata hivyo, Rais Samia anaahidi upatikanaji wa maji wa asilimia 95 mjini na 85 vijijini ifikapo mwaka 2030 na hii ndiyo tofauti ya Rais Samia na marais wengine wengi.