TANGAZO

TANGAZO

DKT. SAMIA AAHIDI MAMBO MAKUBWA 9 AKIWA MTWARA, LIKIWEPO SUALA LA KILIMO NA UFUGAJI


Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amehutubia wananchi wa Mangaka akisisitiza mafanikio yaliyopatikana kupitia ruzuku za pembejeo na mbolea. 

Ameeleza kuwa matumizi bora ya ruzuku yamewezesha ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula.

Aidha, akielezea , uzalishaji wa korosho umeongezeka kutoka tani 15,000 hadi tani 24,000, na kuwaingizia wakulima zaidi ya shilingi bilioni 73. Mazao mengine kama karanga yameongezeka Tani 26,100 yenye thamani bilioni 65 hadi tani 33,170 yenye thamani ya bilioni 82.9, ufuta umeongezeka kutoka tani 1,580 yenye thamani ya bilioni 3.9 hadi tani 11,800 yenye thamani ya bilioni 38.8. na zao la mbaazi limeongezeka kutoka tani 1,130 yenye thamani ya bilioni 1 hadi 5,950 bilioni 10 na milioni 800 zimeingia mkononi kwa wakulima.

 Dkt. Samia amesisitiza kuwa mafanikio haya yamewawezesha wananchi kujenga nyumba bora, kusomesha watoto na kuimarisha maisha yao.

Aidha, miradi ya visima vya umwagiliaji katika maeneo ya Likokona, Lukula na Masugulu ipo hatua za mwisho ili kuongeza uzalishaji wa mazao kwa kilimo cha umwagiliaji.

Kuhusu Mradi Wa Gridi Ya Umeme Kuimarisha Miundombinu Katika sekta ya miundombinu, ameeleza kuwa mradi mkubwa wa gridi ya umeme wenye thamani ya shilingi bilioni 307 ambao unatekelezwa, kwa kujenga njia ya umeme kutoka Songea–Tunduru hadi Masasi, ukiwa na vituo vya kupooza umeme Tunduru na Masasi. 

Ujenzi wa kituo cha Tunduru kimefika 50%. Hii yote ni kuhakikisha Ruvuma inapata umeme bila changamoto. Kuhusu Barabara Na Maeneo Ya Malisho Dkt. Samia amewaahidi wananchi kuendelea kuboresha barabara za lami ndani ya mji wa Mangaka na zile zinazounganisha wilaya na mkoa, pamoja na kujenga madaraja pale panapohitajika. 

Ameeleza kuwa changamoto za wanyama waharibifu kwenye maeneo yanayozunguka misitu ya Lukwila na Lumesule zitapatiwa ufumbuzi.

Aidha, amesisitiza kuwa serikali itaongeza maeneo ya rasmi malisho kwa wafugaji kutoka ekari milioni 3.4 za sasa hadi kufikia milioni 6 Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa Masasi, ameeleza kuwa ruzuku za pembejeo, mbolea na viuatilifu zimeongeza uzalishaji wa mazao, na kuingiza fedha nyingi mikononi mwa wakulima. 

Ameahidi kuendeleza ruzuku hizi pamoja na kutoa chanjo za mifugo kwa wafugaji. 

Aidha, serikali itaendelea kujenga skimu za umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji mara mbili kwa mwaka, sambamba na ujenzi wa kongani za viwanda katika kila wilaya ili kuongeza thamani ya mazao.

Kuhusu Umeme Na Miundombinu Ya Barabara

Katika sekta ya umeme, Dkt. Samia ameeleza kuwa serikali yake inatekeleza mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Ruvuma–Tunduru hadi Masasi, wenye vituo viwili vya kupooza na kusambaza. Aidha, kwenye barabara, tutaendelea kukamilisha kazi tuliyoianza, Barabara ya Mnivata-newala-masasi tutaikamilisha. 

Pia ameahidi kukamilishwa kwa sehemu ya barabara ya Minivata–Mtesa (km 100) kwa kiwango cha lami, pamoja na barabara zingine za mjini Masasi zipitike bila wasiwasi.

Kuhusu Huduma Za Jamii Na Biashara

Kwa upande wa huduma za jamii, Dkt. Samia amesisitiza kuwa serikali ya CCM itaendelea kuhakikisha upatikanaji wa maji safi, kujenga na kukamilisha vituo vya afya na zahanati, sambamba na kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya elimu. 

Aidha, ameeleza kuwa serikali inakusudia kuunganisha bandari ya Mtwara na Bambabay kwa njia ya reli, ili kuongeza fursa za biashara na usafirishaji.

Amewahakikishia wananchi kwamba serikali itabaki karibu na wafanyabiashara wadogo, wakiwemo bodaboda, bajaji na wamachinga, kwa kuwapatia masoko na mitaji kupitia halmashauri.

Kuhusu Huduma Za Kijamii

Dkt. Samia Suluhu Hassan amehutubia wananchi wa Nakapanya, akiahidi kujenga kituo cha afya katika kata ya Namiungo ambacho hakikukamilika awamu iliyopita. Aidha, amesisitiza kuwa vituo vya afya na zahanati ambavyo bado havijakamilika, vitakamilishwa ili kuongeza upatikanaji wa huduma za afya.

Kwenye sekta ya maji, mgombea wa chama cha mapinduzi ameahidi kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata maji safi na salama

Aidha, amesisitiza kuwa umeme sasa umefika vijiji vyote, na hatua inayofuata ni kuunganisha vitongoji vyote.

Kuhusu Kilimo na Umwagiliaji

Dkt Samia ameeleza kuwa serikali itaendeleza ruzuku ya mbolea na pembejeo, pamoja na kujenga skimu za umwagiliaji na mabwawa ili wakulima wazalishe mara mbili kwa mwaka, ukilinganisha na mara moja kufuatia mvua. 

Aidha, amesema kuwa serikali imenunua ndege zisizokuwa na rubani (drones) tano kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za wanyama waharibifu, na zitapelekwa maeneo yenye changamoto kubwa.

Kuhusu Bei Za Mazao

Kwa upande wa bei za mazao, ameeleza kuwa serikali ipo kwenye mazungumzo na masoko makubwa, ikiwemo India, kuhakikisha bei hazishuki zaidi ya asilimia 60 ya bei ya dunia, ili kulinda kipato cha wakulima. 





Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com